HADITH:KAZALIWA AKIWA MZEE
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ
SIMU:0757235417
Hapo kale palikuwapo Nyani aliyekuwa akipenda sana kujisifia kwamba yeye ni mzuri sana kuliko wanyama wote.Kila sehemu alipokwenda alikuwa akijitapa kuwa hakuna atakayeweza kumfikia kwa uzuri alokuwa nao hakuishia hapo bali alikuwa akiwatukana wanyama wenzie na pia hakuacha kusema kuwa yeye yupo katika mabadiliko ipo siku atabadilika na kuwa binadamu “oneni sura yangu na yabinadamu sizinafana,haya manyoya yanapungua kila siku, sikuzaliwa hivi muda si mrefu yataisha kabisa nitakuwa ninangozi nyororo kama ya binadamu,angalieni jinsi ninavyotembea sio kama nyinyi mnavyokuwa mkiinamisha migongo ninafikiri ni mwezi ujao tu nitajua kutembea kwa miguu miwili kistaimilivu yaani kama binadamu,nanikiwa binadamu hao binadamu watanikoma em angalieni haya mashimo kwenye mashavu na nikitabasamu mwanya unaonekana kwenye meno oneni iii iii..”na hivyo ndivyo alivyokuwa akiwatambia wanyama wenzake.Baadhi ya wanyama waliamini kuwa hayo anayoyasema Nyani niyaukweli wengi wao walinyong’onyea huku wakimshutumu Mwenyezi Mungu kuwa anaupendeleo.
Siku moja taarifa zikamfikia kuwa Nguruwe amezaa,punde tu baada ya kupata habari hiyo akaenda moja kwa moja kumpa hongera,mara akafika na maongezi yao yakawa hivi:
“hodi hodi jamani”
“karibu!”
“nshakaribia!nimekuja kukupa hongera nasikia umezaa watoto kumi na mbili”
“ndio! mume wangu ananigombeza eti kwanini kipindi hiki nimezaa watoto wachache anadai eti siku hizi maisha magumu kwahiyo itabidi tuwale wote tubakize mmoja”
“anachoseema mume wako ni sahihi na siku nikiwa binadamu nitawaelekeza binadamu njia hii ya kitaalamu ya uzazi wa mpango”punde tu wale watoto wakaletwa.
“watoto wenyewe ndo hawa?”
“ndio!kwani kunatatizo?”
“mmh!shoga yangu watoto wenyewe mbona wanasura mbaya kiasi hiki!”
“mmmh!hata mimi sijui labda wamefuata sura ya baba yao”
“tatizo lenu watoto mnawazalia kwenye matope kiasi kwamba wakati mtoto anatoka anakutana na harufu mbaya kwahiyo anakunja sura sasa ile mikunjo inabakia milele..em toeni hapa vitoto vyenu nsije nikaota usiku majinamizi!”wakati huwo Nyani anaongea hivyo alikuwa anainuka na kuondoka huku akimuacha Nguruwe katika simanzi kubwa!”
Siku nyingine tena zikamfikia taarifa kuwa Mamba ametotoa vitoto kumi,akakwea matawi mpaka akamfikia Mamba ambapo yupo na wanae ila kwa kuhofia usalama wake akabaki juu ya mti halafu ndo akaanza uchokozi wake “yaani nilijua tu nikija hapa sitoacha kukusikitikia em jiangalie kwenye maji jinsi unavyofanana yaani unatisha,mimi nigekuwa wewe nisingekuwa natoka kwenye maji labda usiku ambapo wanyama wengine hawataniona,angalia sasa hiyo sura yako mbaya umeambukiza hadi wanao,hiyo sura ukiuangalia moto si unazimika,najua unatamani kuwa mimi lakini ndo haiwezekani pole!”Mamba alivyoona kelele zimezidi akaamua kuzama ndani ya maji huku akimuacha Nyani maneno yakizidi kumtoka bila mpangilio.
Haaya sasa mara nae Nyani akapata mimba ngoja aanze kuzunguka huku na kule akitamba yaani kama kawaida yake “jamani ee wakati ndo umekaribia sasa muda sio mrefu nitakuwa sio mwenzenu tena hiki kiumbe nilichonacho tumboni kikitoka ndo mtaniamini na kuniheshimu kwasababu kitatoka kinafanana moja kwa moja na binadamu na kikiwa cha kike mtanikoma kitakua kirembo halafu wanadamu watakiona watakipenda na kikiolewa na binadamu bhasi kukaa porini itakuwa ndo kwaheri!”wanyama wameshachoka kusikiliza stori za Nyani hivyo wakaamua kuendelea shughuri zao.
Siku ya kuzaa nyani wanyama karibu wote walijitokeza ili kushuhudia maajabu jinsi nyani atakavyo zaa mtoto anaefanana sawa kabisa na binadamu.Punde tu baada ya Nyani kuzaa mara vicheko vinaanza kusikika mara wengine wakimzomea huku wakisema MTOTO KAZALIWA AKIWA MZEE,HUYO NI MWANAO AU BABU YAKO!huku wengine wakimkejeri kwa kumwambia “endelea kusukuma pengine binadamu kajificha humo tumboni anamuogopa huyo babu alotangulia”.Ndo maana mpaka leo Nyani akimuona mnyama anapita yeye anajifanya anamtoa chawa mwanae kumbe anaona aibu,hadith yetu nzuri imeishia hapo!!!!!

No comments:
Post a Comment