Monday, January 26, 2015

ADVERTISE AND PROMOTE YOUR BUSINESS with THE BRIGHT FUTURE INTERTAINMENT ....CALL 0718868152 for more information

Wednesday, March 12, 2014



SIMULIZI:MAITI YA LETI
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ

“Leti unajua utaniletea matatizo!”
“Wasiwasi wako nini wakati unajua yule bwege kurudi hapa ni mpaka jumatatu”
“Hata kama kwanini lakini muda huu jua linawaka kabisa Mama mwantum si atajua juu ya mahusiano yetu”
“Mimi sio mtoto mdogo bhana! Huyo Mama Mwantumu unaemzungumzia kwanza hayupo tokea  asubuhi kapigiwa simu na dada yake Yule wa Mbagala kaenda kumuuguza nasikia anaumwa hoi bin taaban na funguo zake kaniachia hizi hapa yaana hata ukiamua tukafanyie ndani kwake twaweza kwenda! Au ndo ushaanza kunichoka na wewe?”
“Sizani kama naweza kukuchoka maana kila siku unamambo mapya haaya leo unajipya gani?”
“Leo utapagawa!embu washa redio usije ukakusanya watu hapo dirishani”
Nikainuka taratibu kutoka pale kitandani na kisha kuzipiga hatua chache mpaka nilipofika karibu na sabufa na nikaliwasha likiwa linanguruma nikachomoa flash kutoka kwenye kibegi changu ambacho huwa ninatunzia Laptop na baada ya hapo nikaichomeka ile flash kwenye Sabufa moja kwa moja mziki mnene ukaanza kurindima ndani ya chumba changu.
Wakati nainuka na kusimama wima nikatupa macho kitandani,nilichokiona kilinifanya nishindwe kabisa kuyaondoa au kuyafumba macho na kitu chenyewe sio kingine ni mtoto Letisia kwa jinsi alivyokuwa amejiachia pale kitandani.Wakati huwo alikuwa kava kangamoja tu halafu miguu kaitanua kiasi cha mimi kuweza kupenyeza macho na kuchungulia kabati yake,taratibu nikiinua macho yangu nagundua kuwa yupo kifua wazi kama haitoshi alikuwa akiitumia mikono yake kujitomasa taratibu kabisa wakati anafanya kitendo hicho alikuwa akiniangalia kwa jicho la huba na mara anaanza kujiliza kimahaba.
Msisimko wa ghafla ukaanza kuenea kila sehemu ya mwili wangu kuanzia kichwani ambapo hadi nywere zilinisimama mapigo ya moyo nayo yakaanza kwenda mbio tena kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba nacho kirungu changu kikasimama wima na kuanza kumtafuta mwizi  sikujua nilifika vipi pale kitandani na hapo nikaanza kupenyeza mkono wangu katikati kabisa ya mapaja yake mara redio ikazima ghafla!

Saturday, February 22, 2014

KARUMANZIRA

HADITHI:KARUMANZIRA
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ

SIMU:0757235417
Hapo zamani za kale palitokea mvua kali sana ilyiosababisha maafuriko makubwa na yaliodumu kwa muda mrefu sana katika maeneo mengi sana hasa nyanda za juu mashariki mwa Tanzania.Mvua hizo zilijulikana kama EL'NINO.

Maafuriko hayo yalisababisha uharibifu mkubwa sana wa mali za watu na mali asili za nchi,pia kutokana na kudumu kwa muda mrefu mazao na miti mingi ilioza na kuteketea.Punde tu baada ya kipindi cha maafuriko kupita pakatokea ukame wa hali ya juu kama waswahili wasemavyo palipo na ukame hapakosi njaa basi watu wakaanza kuhama katika maeneo yao kwaajiri ya kuzunguka huku na kule ili kutafuta chochote cha kukidhi mahitaji yao.

Pengo ni mwanume mwenye mtoto mmoja na anaishi katika kijiji kimoja ambacho nacho kiliathirika zaidi na ukame, kijiji hicho kilijulikana kama Kigimbi.Akiwa kama baba wa familia akajaribu kuangaika huku nakule ili kuweza kuangalia kama anaweza kupata japo kibarua lakini hali ikawa tofauti kwa maana ya kwamba hakufanikiwa kupata.

Siku moja akiwa yupo sebuleni kwake amekaa kwenye kiti huku amejishika tama akiwa anajaribu kuishughurisha akili yake kwa kufikiria ni jinsi gani ataiendesha familia yake mara ghafla anapata wazo la kijasiliamali.Taratibu akaanza kutabasamu kwa kuamini wazo lile huwenda likayabadili maisha yake.

Haraka haraka akatoka nje nakuanza kujenga kibanda mara akaingia msituni na kutafuta tunguri pamoja vibuyu,pia akaandaa mashuka yenye rangi nyekundu na nyeusi na kisha akayatumia kujifunga na mengine kuzungushia kibanda chake.

Alipomaliza maandalizi ya kibanda hicho akaandaa bango kubwa lenye maandishi yafuatayo:MGANGA KUTOKA SUMBAWANGA ANATIBU MARADHI YOTE YA KIAFYA PAMOJA NA MAMBO MENGINE KAMA KUONGEZA AKILI,KUPENDWA,BAHATI BILA KUSAHAU HESHIMA YA NYUMBA KWA WANAUME,chini kabisa akamalizia kwa kuandika DOKTA PINGU au KARUMANZIRA.Akalipachika bango hilo karibu kabisa na barabara kubwa kisha kurudi kwenye kibanda chake na kusubiri wateja,mara anamsikia mwanamke mmoja anabisha hodi:


Friday, February 21, 2014

KAZALIWA AKIWA MZEE

HADITH:KAZALIWA AKIWA MZEE
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ

SIMU:0757235417

Hapo kale palikuwapo Nyani aliyekuwa akipenda sana kujisifia kwamba yeye ni mzuri sana kuliko wanyama wote.Kila sehemu alipokwenda alikuwa akijitapa kuwa hakuna atakayeweza kumfikia kwa uzuri alokuwa nao hakuishia hapo bali alikuwa akiwatukana wanyama wenzie na pia hakuacha kusema kuwa yeye yupo katika mabadiliko ipo siku atabadilika na kuwa binadamu “oneni sura yangu na yabinadamu sizinafana,haya manyoya yanapungua kila siku, sikuzaliwa hivi muda si mrefu yataisha kabisa nitakuwa ninangozi nyororo kama ya binadamu,angalieni jinsi ninavyotembea sio kama nyinyi mnavyokuwa mkiinamisha migongo ninafikiri ni mwezi ujao tu nitajua kutembea kwa miguu miwili kistaimilivu yaani kama binadamu,nanikiwa binadamu hao binadamu watanikoma em angalieni haya mashimo kwenye mashavu na nikitabasamu mwanya unaonekana kwenye meno oneni iii iii..”na hivyo ndivyo alivyokuwa akiwatambia wanyama wenzake.Baadhi ya wanyama waliamini kuwa hayo anayoyasema Nyani niyaukweli wengi wao walinyong’onyea huku wakimshutumu Mwenyezi Mungu kuwa anaupendeleo.

Siku moja taarifa zikamfikia kuwa Nguruwe amezaa,punde tu baada ya kupata habari hiyo akaenda moja kwa moja kumpa hongera,mara akafika na maongezi yao yakawa hivi:
“hodi hodi jamani”
“karibu!”
“nshakaribia!nimekuja kukupa hongera nasikia umezaa watoto kumi na mbili”
“ndio! mume wangu ananigombeza eti kwanini kipindi hiki nimezaa watoto wachache anadai eti siku hizi maisha magumu kwahiyo itabidi tuwale wote tubakize mmoja”
“anachoseema mume wako ni sahihi na siku nikiwa binadamu nitawaelekeza binadamu njia hii ya kitaalamu ya uzazi wa mpango”punde tu wale watoto wakaletwa.
“watoto wenyewe ndo hawa?”
“ndio!kwani kunatatizo?”
“mmh!shoga yangu watoto wenyewe mbona wanasura mbaya kiasi hiki!”
“mmmh!hata mimi sijui labda wamefuata sura ya baba yao”
“tatizo lenu watoto mnawazalia kwenye matope kiasi kwamba wakati mtoto anatoka anakutana na harufu mbaya kwahiyo anakunja sura sasa ile mikunjo inabakia milele..em toeni hapa vitoto vyenu nsije nikaota usiku majinamizi!”wakati huwo Nyani anaongea hivyo alikuwa anainuka na kuondoka huku akimuacha Nguruwe katika simanzi kubwa!”

Siku nyingine tena zikamfikia taarifa kuwa Mamba ametotoa vitoto kumi,akakwea matawi mpaka akamfikia Mamba ambapo yupo na wanae ila kwa kuhofia usalama wake akabaki juu ya mti halafu ndo akaanza uchokozi wake “yaani nilijua tu nikija hapa sitoacha kukusikitikia em jiangalie kwenye maji jinsi unavyofanana yaani unatisha,mimi nigekuwa wewe nisingekuwa natoka kwenye maji labda usiku ambapo wanyama wengine hawataniona,angalia sasa hiyo sura yako mbaya umeambukiza hadi wanao,hiyo sura ukiuangalia moto si unazimika,najua unatamani kuwa mimi lakini ndo haiwezekani pole!”Mamba alivyoona kelele zimezidi akaamua kuzama ndani ya maji huku akimuacha Nyani maneno yakizidi kumtoka bila mpangilio.


Haaya sasa mara nae Nyani akapata mimba ngoja aanze kuzunguka huku na kule akitamba yaani kama kawaida yake “jamani ee wakati ndo umekaribia sasa muda sio mrefu nitakuwa sio mwenzenu tena hiki kiumbe nilichonacho tumboni kikitoka ndo mtaniamini na kuniheshimu kwasababu kitatoka kinafanana moja kwa moja na binadamu na kikiwa cha kike mtanikoma kitakua kirembo halafu wanadamu watakiona watakipenda na kikiolewa na binadamu bhasi kukaa porini itakuwa ndo kwaheri!”wanyama wameshachoka kusikiliza stori za Nyani hivyo wakaamua kuendelea shughuri zao.

Siku ya kuzaa nyani wanyama karibu wote walijitokeza ili kushuhudia maajabu jinsi nyani atakavyo zaa mtoto anaefanana sawa kabisa na binadamu.Punde tu baada ya Nyani kuzaa mara vicheko vinaanza kusikika mara wengine wakimzomea huku wakisema MTOTO KAZALIWA AKIWA MZEE,HUYO NI MWANAO AU BABU YAKO!huku wengine wakimkejeri kwa kumwambia “endelea kusukuma pengine binadamu kajificha humo tumboni anamuogopa huyo babu alotangulia”.Ndo maana mpaka leo Nyani akimuona mnyama anapita yeye anajifanya anamtoa chawa mwanae kumbe anaona aibu,hadith yetu nzuri imeishia hapo!!!!!

HADITHI YA LEO

HADITH:SUNGURA MZAA SIMBA
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ
SIMU:0757235417,0683173005,0657098244


Hapo zamani palikuwepo Sungura mwenye rangi nyeupe na michoro kama michirizi ya rangi nyeusi pia maeneo ya tumboni kulitapakaa rangi ya kahawia kwakweli alikuwa ni Sungura wa aina yake.Rangi za manyoya yake zilimfanya avutie sana hasa  kwa kila kiumbe aliye mtazama.Sungura huyo alipewa jina Malika kutokana na uzuri alikuwa nao.
Siku moja akiwa matembezini akarushiwa kiazi,taratibu akaikota na kuanza kuangaza ninani kampatia zawadi hile ya kupendeza lakini hakuweza kuona mtu,mara ghafla anasikia sauti nzito kutoka kichakani ikiimba:

chakacha si kachakuchu,sipendi vyenye uchachu,
usinone mwenye uchu,wananita palakuchu,
nimependa zako chuchu,nipepojapo kiduchu,
sipendi kupiga puchu,chakacha ni palakuchu,


Baada ya kusikiliza kwa makini kabisa huku akizipiga hatua za taratibu kuelekea itokako sauti hiyo ghafla anatokea sungura dume anaejulikana kwa jina la Koba.Hali ile ilimshangaza Malika ikabidi asimame huku akimtazama Koba,wakati huo huo nae Koba akaamua aitumie nafasi ile kujinadi "Wananiita Koba ukipenda Baba lao,usihofu kiazi hicho ni zawadi yako nimekinunua bei mbaya,nimepanda milima na mabonde kwaajiri ya kukutafutia zawadi yako hiyo yote hayo kutokana na kwamba wewe ndo mwanamke wa ndoto zangu,nusu ni pigwe jiwe na binadamu kwasababu ya kiazi hicho hivyo naomba ukipokee na unipokee na mimi pia katika moyo wako"

Baada ya kuyaongea hayo mara nae Malaika akaanza kuzipiga hatua na kumkalibia kabisa Koba na kisha akaanza kuongea taratibu huku akimzunguka "em jiangalie wewe na kisha uniangalie mimi hivi unaona tunaendana,kwahiyo sura yako hiyo ka unatumbuliwa jipu si tutazaa majini,duh!nilikuwa sijaona tumiguu aye ye ye hii ni miguu au tambi hivi unaweza kutembea kweli em tembea nikuone,halafu yaani umeamua kunidharirisha kiasi hiki eti zawadi kiazi chenyewe umeiba sasa kwa taarifa yako mimi nshawahiwa muda si mrefu Simba ananioa hivyo kwa usalama wako changanya milonjo yako upotee mbele yangu."akamrushia kiazi chake kisha kuendelea na safari ya huku akimuacha Koba katika hali ya huzuni.

Siku nyingine akiwa katika mizunguko yake ndipo anakutana na sungura mwingine dume aitwae Chuma akiwa kavaa suti maridadi kabisa huku mkononi kashika cheni ya ghahabu .Kwa dharau zake akampita bila hata ya kumsalimia ila ghafla anakamatwa mkono huku akiambiwa “najua hunifahamu ila mimi ninakufahamu,naimani iwapo ukinifahamu utajuta kwanini umepita bila ya kunisalimia na ninauwezo wa kukufanya chochote na nisifanywe chochote na yeyote hivyo kuwa mpole na unisikilize kwa makini”wakati huo Malikia alikuwa akijaribu kujinasua ila anazidiwa nguvu ndipo nae Chuma akazidi kutamba kwa mbwembwe  “najua unajijua na kila mtu anajua ya kuwa wewe ni mrembo kuliko sungura wote msituni hapa na unafaa kuwa na mtu kama mimi.Kwautanbulisho tu mimi naitwa Mfaulme Chuma ninamiliki shamba kubwa sana la karoti lenye jumla ya mita za eneo mbili na nusu sasa nahitaji uwe malikia wangu”mara ghafla unasikika muungurumo wa simba kwa haraka haraka Mfalme Chuma anamwachia Malikia na kujificha nyuma ya mti anasikia kama anafuatwa kwa nyuma kwahofu na uoga uliokithiri akajika anageuka kwa harakaharaka kuangalia mara ameshakaribiwa na Malaika: