Saturday, February 22, 2014

KARUMANZIRA

HADITHI:KARUMANZIRA
MTUNZI:ABDULMALIK SIRAJ

SIMU:0757235417
Hapo zamani za kale palitokea mvua kali sana ilyiosababisha maafuriko makubwa na yaliodumu kwa muda mrefu sana katika maeneo mengi sana hasa nyanda za juu mashariki mwa Tanzania.Mvua hizo zilijulikana kama EL'NINO.

Maafuriko hayo yalisababisha uharibifu mkubwa sana wa mali za watu na mali asili za nchi,pia kutokana na kudumu kwa muda mrefu mazao na miti mingi ilioza na kuteketea.Punde tu baada ya kipindi cha maafuriko kupita pakatokea ukame wa hali ya juu kama waswahili wasemavyo palipo na ukame hapakosi njaa basi watu wakaanza kuhama katika maeneo yao kwaajiri ya kuzunguka huku na kule ili kutafuta chochote cha kukidhi mahitaji yao.

Pengo ni mwanume mwenye mtoto mmoja na anaishi katika kijiji kimoja ambacho nacho kiliathirika zaidi na ukame, kijiji hicho kilijulikana kama Kigimbi.Akiwa kama baba wa familia akajaribu kuangaika huku nakule ili kuweza kuangalia kama anaweza kupata japo kibarua lakini hali ikawa tofauti kwa maana ya kwamba hakufanikiwa kupata.

Siku moja akiwa yupo sebuleni kwake amekaa kwenye kiti huku amejishika tama akiwa anajaribu kuishughurisha akili yake kwa kufikiria ni jinsi gani ataiendesha familia yake mara ghafla anapata wazo la kijasiliamali.Taratibu akaanza kutabasamu kwa kuamini wazo lile huwenda likayabadili maisha yake.

Haraka haraka akatoka nje nakuanza kujenga kibanda mara akaingia msituni na kutafuta tunguri pamoja vibuyu,pia akaandaa mashuka yenye rangi nyekundu na nyeusi na kisha akayatumia kujifunga na mengine kuzungushia kibanda chake.

Alipomaliza maandalizi ya kibanda hicho akaandaa bango kubwa lenye maandishi yafuatayo:MGANGA KUTOKA SUMBAWANGA ANATIBU MARADHI YOTE YA KIAFYA PAMOJA NA MAMBO MENGINE KAMA KUONGEZA AKILI,KUPENDWA,BAHATI BILA KUSAHAU HESHIMA YA NYUMBA KWA WANAUME,chini kabisa akamalizia kwa kuandika DOKTA PINGU au KARUMANZIRA.Akalipachika bango hilo karibu kabisa na barabara kubwa kisha kurudi kwenye kibanda chake na kusubiri wateja,mara anamsikia mwanamke mmoja anabisha hodi:



"hodii hodii"
"karibu karibu vua viatu vyako halafu ingia kinyumenyume(kwa sauti nzito)
karibatokora karitokora kitororo kitokororo iyaaaaku nimekuona tokea unainza safari yako najua unasumbuliwa na tumbo shokorokoro shoko yyyyyyyeebaaah hapa ndo umefika kwa karumaaanzira hakuna kinachoshindikana"
"ila mganga mimi sisumbuliwi na tumbo nasumbuliwa na mgongo!"
"ssssshukurree sssshukurreeee wewe mama hukunisikia vizuri mimi sijasema tumbo nimesema tumbiii hiyo ni kwa lugha za mizimu kiswahili chake ni mgongo..."
Kwa hamaki kabisa yule mama akaamua kumwambia Mganga Karumanzira
“Basi nisaidie maana nimezunguka kwa wataalamu tofauti tofauti lakini sija fanikiwa”
“kaaaaraareee karaaarre maaassaraalee sasa mama wazee wamekwisha sikiliza shida yako na wamenituma nikwambie ya kwamba utapona kabisa sasa kwakuwa tatizo lako ni la kiafya basi litatibiwa kupitia dawa za miti shamba hivyo basi mimi naenda kukutafutia dawa lakini nikirudi nikute umesha wapoza wazee wangu kwa chochote”
“kama shilingi ngapi?”
“hapo ni chochote ila nikuanzia shilingi elfu tano”
Mganga Karumanzira akatoka nje na kuzunguka nyuma kidogo ya nyumba yake kisha akaanza kukata baadhi ya majani ya muembe akachanganya na majani ya mpapai akachanganya pia majani ya mparachichi,akaya twanga majani hayo na kisha kuyaweka kwenye kachupa.
“sasa mama dawa yako hii hapa”
“ahsante daktari sasa naitumiaje?”
“mmmmm mmm tumia nne mara moja ila ukiona unaharaka ya kupona basi utatumia tano mara moja kwa kutumia kijiko kidogo”


Yule mama akaondoka na kumuacha Karumanzira akikichungulia chungu chake ndipo anagundua kuwa ameachiwa shilingi elfu kumi akafurahi sana na akaona hiyo biashara inalipa.Karumaanzira akanogewa kabisa akawa anawadanganya wagonjwa ilimradi tu apate chochote,mchezo huwo hatari ulifanya baadhi ya wagonjwa kupeza maisha yao.
Siku moja akiwa yumo kwenye kakibanda kake mara akaja baba mmoja alipo mkaribisha akamuuliza shida yake.
“Mganga nisaidie maana mimi sikuhizi biashara zangu haziendi kabisa nahisi ninamkosi”
“cchhakaka rrraaba rrruba ssssukkka ssssaaabbbba ssssaba shakassssuka nyota yako imechafuriwa,umefanya kitu cha maana kuja kuwaona wazeee maana wafanya biashara wenzako wamepanga kukutoa duniani kabbbisa “
“eee!sasa utanisaidiaje Mganga?”
“nitakusaidia ila inabidi ulete samaki mwenye mwanya,jasho la nyoka,sisimizi mwenye matege,pamoja na jino la kiloboto.”
“mmmmh hivyo vitu kwakweli siwezi kupata ila chukua hii laki mbili nafikiri itatosha kutafutia vitu hivyo”
“usinipe mimi hiyo pesa ya wazee wape wao wwwwweka hiyo pesa kwenye hicho chungu shaaaakarrrubah naaam naaam wazee wamekubari ombi lako nisubirie hapa naenda kukutafutia dawa.”
Kama kawaida akaenda kuchanganya majani yake na kisha kyaponda vizuri baada ya kuyaweka kwenye chupa akajanayo kibandani.Akamkabidhi yule mteja kale kachupa na maongezi yao yakawa hivi:
“sasa chuku hii dawa inabidi utafune kila unapoamka na kila unapotaka kulala”
“duh ama kweli inamaana mimi nimekuwambuzi”
“kaaaatiirrrrabah unadiriki kuibishia mizimu”
“acha uchizi wewe mizimu haija kwambia unilishe majani ya mpera na muembe”
“ntakugeuza dodoki”
“thubutu!kwanza upo chini ya ulinzi taperi mkubwa”Mara ghafla akaona maaskari zaidi ya kumi wamezunguka kibanda chake akaamua kuwa mpole kama maji mtungini,basi alipofikishwa mahakani akahukumiwa kifungo cha miaka miwili jera na hadithi yetu imeishia hapa.

No comments:

Post a Comment